Alhamisi, 8 Agosti 2013

*HEKA HEKA ZA MTAA WA KONGO DAR NA MAANDALIZI YA SIKUKUU YA IDD EL FITRI

 Wakazi wa Jijini Dar es Salaam, wakiwa wamefurika katika Mtaa wa Kongo Jijini Dar es Salaam, leo wakisaka mahitaji ya nguo, viatu, urembo na mengineyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sikukuu ya Iddi-el Fitri, inayotarajiwa kusherehekewa mwishoni mwa wiki hii kutegemea na kuandama kwa mwezi. 
  Wakazi wa Jijini Dar es Salaam, wakiwa wamefurika katika Mtaa wa Mchikichini Jijini Dar es Salaam, leo wakitafuta viatu, mengineyo ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Sikukuu ya Iddi-el Fitri, inayotarajiwa kusherehekewa mwishoni mwa wiki hii kutegemea na kuandama kwa mwezi. 
 Wakichagua nguo Mtaa wa Kongo.
 Kina Mama wa jijini Dar es Salaam, wakichagua nguo aina ya Madela Mtaa wa Kongo.
 Wakazi wa Jijini dar wakichagua nguo za kiume za watoto wao kwa ajili ya Sikukuu ya Idd el Fitri.
 Akichagua urembo, haikuweza kufahamika kama jamaa huyu ni muuzaji ama alikuwa akimchagulia urembo 'naniliu' wake...
 Jamaa naye akijipima kofia akijiandaa na swala ya Idd.....
 Mtaa wa Kongo Hakufai leo usiende....................
Kongo hiyo hakuna hata njia hata watu tu hipishana kwa tabu

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni